Hayo yamesemwa na Mkuu wa chuo hicho Bw.Joseph Mayagila wakati akifungua semina ya ujasiriamali ambayo ilifanyika kwa siku tatu chuoni hapo kuanzia tarehe 1 mpaka tarehe 3 Octoba mwaka huu chuoni hapo.
Bw.Mayagila ameongeza kuwa wanafunzi wengi hawana tabia ya kujiwekea akiba katika fedha ambazo wanatumiwa na wazazi wao kwa ajili ya matumizi na kuwaasa wanafunzi hao wawe wanajiwekea akiba kwa maendeleo yao.
Katika semina hiyo walimu wa chuo hicho waliyoa mada mbalimbali zikiwemo za mpango wa biashara,miongozo ya mjasiriamali,namna ya kutathmini biashara pamoja na nyingine nyingi ambapo wanafunzi wote wa chuo hicho walishiriki.
Pia ili kuongeza vionjo katika semina hiyo kulikuwepo na burudani mbalimbali ambapo wanafunzi walipewa fursa ya kuonyesha vipaji vyao mbele wanafunzi wenzao na burudani hizo ni pamoja na kuimba pamoja na vichekesho.
Nao wanafunzi wa chuo hicho wamesema kuwa wamefurahishwa na uwepo wa semina hiyo kwa sababu imewafunza mambo mbalimbali juu ya ujasiriamali ambayo hawakuwa wakiyafahamu.
Akizungumza ili kuhitimisha semina hiyo makamu mkuu wa chuo Bw.Elifuraha Samboto amewataka wanafunzi kuwaheshimu walimu na vilevile wawe na tabia ya kjisomea.
Bw.Samboto alimaliza kwabkuwashukuru walimu na wanafunzi kwa ushiriki wao katika semina ya jasiriamali.









