Showing posts with label KIJAMII. Show all posts
Showing posts with label KIJAMII. Show all posts
Friday, June 6, 2014
MTOTO WA MAREHEMU TYSON "SONIA" ATOA WOSIA MZITO KUHUSU KIFO CHA BABA YAKE, SIKILIZA SAUTI YAKE HAPA
Juzi simanzi ma majonzi vilitawala katika viwanja vya Leaders Club
wakati mamia ya watu walipokuwa wakiaga mwili wa muongozaji wa filamu na
vipindi vya televisheni, George Tyson aliyefariki katika ajali ya gari.
Moja kati ya matukio yaliyowatoa machozi mamia ya watu waliohudhuria
katika tukio la kumuaga Tyson, ni pale mtoto wake wa kike aitwae Sonia
alipokuwa akitoa neno/ujumbe wa kumuaga baba yake.
Sonia aliongea kwa majonzi maneno yaliyosababisha watu wengi watokwe machozi.
“You were kind na rafiki yangu kipenzi. Ulikuwa mtu ambaye ni
rahisi kuongea nae na kunielewa. Daima ulikuwa unanitunza na kunidekeza.
Na mara ya mwisho kuonana na wewe wiki iliyopita ulinambia ni jinsi
gani nimekufanya uwe pride na mimi. And moreover I sing…I take a breath
away. Na ninakuahidi, sitaacha kuimba kwa ajili yako. Nataka ufahamu
kwamba nitakupenda milele. I will always Love You dad. Rest In Peace.”
Sonia ni mtoto wa marehemu aliyempata na muigizaji Monalisa ambaye pia ni mtangazaji wa 100.5 Times Fm.
credit: eddy blog
Na Flaviana makawia
Tajiri adaiwa kumng’ata, kumchoma pasi mtumishi wake kwa miaka mitatu
Dar es Salaam. Mfanyakazi wa ndani, Yusta Lucas (20) amekumbana na masahibu yanayofanana na yale ya mtoto Nasra Mvungi (4) aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka karibu minne huko Morogoro. Huyu amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam akiuguza majeraha yanayotokana na kuteswa na kufungiwa ndani kwa miaka mitatu.
Binti huyo, mwenyeji wa Mkoa wa Tabora, katika
Kijiji cha Kampala amedai kuwa amekuwa akiteswa na kufungiwa ndani ya
nyumba na tajiri yake, Amina Maige wa Mwananyamala, Kwa Manjunju katika
kipindi chote hicho. Amina anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha
Oysterbay kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba OB/RB/9967/2014.
Akisimulia masahibu yaliyompata akiwa katika Wodi
Namba Tatu ya hospitali hiyo, Yusta alisema: “Nililetwa Dar es Salaam
mwaka 2010 kufanya kazi za nyumbani baada ya bosi wangu (Amina) ambaye
ni binamu yangu kuzungumza na mama yangu na kuniomba nije kumsaidia kazi
ndogondogo.”
Alisema aliishi vizuri na mwajiri wake huyo,
lakini mwaka 2012 ndipo mambo yalipoanza kubadilika akidai kuwa Amina
alianza kumwadhibu kwa kumng’ata na kumchoma kwa pasi kila alipomtuhumu
kutokufanya kazi zake vizuri.
“Alikuwa akinichapa na kuning’ata sehemu
mbalimbali wakati mwingine usoni, pia kunichoma kwa pasi yenye moto kila
aliponituhumu kutokufagia au kupiga deki vizuri.”
Hakuwahi kupelekwa hospitali
Alisema licha ya kupata vidonda kutokana na adhabu
hizo, mwajiri wake huyo hakuwahi kumpeleka hospitali na pale alipoona
hali ni mbaya alimnunulia dawa... “Tunaishi wawili tu baada ya kuondoka
mumewe na mtoto wake kumpeleka shule ya bweni... niliugulia hadi
nikapona bila mtu mwingine kufahamu.”
“Akienda kazini anafunga geti na kunikataza
kufungua hata kama mtu atagonga… sokoni nilikuwa naenda siku ambazo yeye
yupo tu na huwa akiniamrisha niende haraka na kurudi pasipo kuzungumza
na mtu yeyote.”
Alisema mwajiri wake huyo alikuwa akituma pesa za
mshahara wake kwa mama yake akisema ndiye anayepaswa kulipwa, jambo
ambalo anadhani limemfanya mama yake kuhisi mwanaye yuko katika mikono
salama... “Kila alipotuma alipiga simu na kunipa niongee na mama
kuhakikisha kama zimefika huku akinisimamia na baada ya hapo anachukua
simu.”
Ataka kurudi kwao
Binti huyo ambaye sehemu kubwa ya mwili wake ina
alama za kung’atwa meno na majeraha ya kuchomwa na pasi, alisema:
“Ninaomba mtu yeyote mwenye hela, nataka nikitoka hapa hospitali nirudi
Tabora kwa mama. Nina shaka na maisha yangu hapa kwa huyu mama… sitaki
tena kubaki Dar es Salaam kutokana na mateso ninayoyapata.
credit: mwananchi
Na Dorcas Mdemu
credit: mwananchi
Na Dorcas Mdemu
Wednesday, April 16, 2014
KUHUSU BOMU LA ARUSHA POLISI WATANGAZA BINGO KWA ATAKAYEFANIKISHA KUKAMATWA KWA WALIPUAJI NIGHT PARK
Friday, March 21, 2014
Mwanafunzi wa chekechea wa miaka 6 alawitiwa Iringa,mmoja akamatwa na misokoto wa bhangi
source:PRINCEMEDIA TZ BLOG










