NICE MEDIA WORKS

KWA WAIMBAJI WA INJILI

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, December 4, 2013

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUJENGA MAZOEA YAKUJISOMEA VITABU MBALIMBALI!!

Mkurugenzi wa redio faraja Bw.Simeo Makoba akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari na Utangazaji.


Mkurugenzi wa kituo cha redio faraja Bw.Simeo Makoba amewataka waandishi wa habari kujenga mazoea ya kujisomea vitabu pamoja na kusikiliza vyombo mbalimbali vya habari ili kujua taarifa zinazoendelea hapa nchini na nje ya nchi.

MAHAFALI YA SABA KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA (AJTC) KUFANYIKA HIVI KARIBUNI!



Maafali ya saba katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) yanatarajiwa kufanyika hivi  kwa na lengo la kuwaaga wanafunzi wanaohitimu ngazi ya Cheti na Stashahada katika tasnia ya habari.

Kwa mujibu wa  Mlezi wa wanafunzi wa chuo hicho Bw.Andrew Ngobole alisema kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo anatarajiwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Nyirenda Munasa. 



 Mahafali hayo yanatarajia kufanyika mnamo tarehe sita (6) mwezi wa kumi na mbili katika ukumbi wa PPS ulioko maeneo ya Mbauda mkoani Arusha ikiwa ni mahafali ya saba tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Tuesday, December 3, 2013

WANANCHI WAASWA KUJENGA MAZOEA YAKUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA!!

Katika kuelekea kuadhimisha siku ya ukimwi duniani, meya wa manispaa ya jiji la Arusha Bw. Gaudens Lyimo amewataka wananchi kujenga mazoea ya kupima afya zao kila wakati ili kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi

Sunday, December 1, 2013

KAULI MBIU YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI:“TANZANIA BILA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU, VIFO VITOKANAVYO NA UKIMWI NA UBAGUZI NA UNYANYAPAA INAWEZEKANA”

Siku ya UKIMWI Duniani iliasisiwa rasmi na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) mwaka 1998 na imeendelea kuadhimishwa kila mwaka ifikapo Desemba mosi kwa uratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI (UNAIDS). 

WANAHABARI WATAKIWA KUWAFICHUA WANAOUZA DAMU MAHOSPITALINI!!

Mtaalamu  kutoka tume ya uchangiaji damu salama Nchini Bw.George Chambo akitoa utambulisho mfupi wa msafara aliofuatana nao.

Katika kuhakikisha kunakuwepo na damu ya kutosha katika benki ya damu mahospitalini waandishi wa habari wametakiwa kuwa msitari wa mbele kuchangia damu pamoja na kuwafichua wale wote wanaohusika  kuuza damu kwa wagonjwa.

Wito huo umebainishwa na mtaalamu wa Mpango wa Taifa wa  kuchangia damu salama  Bw.George Chambo alipoongea na wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa habari na utangazaji Arusha katika zoezi  lililofanyika la uchangiaji wa damu.

Thursday, November 21, 2013

WANASHERIA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KENYA,RWANDA NA UGANDA WAFULIWA KESI!!


Wakili Jimmy obedi akiwa anakabidhi nyaraka za kesi dhidi ya serikali za
Kenya,Rwanda na Uganda,kwa Afisa masijala wa mahakama ya Afrika ya
mashariki Boniface Ogoti jana.kulia ni mmoja wa walalamikaji Ally msangi.
 Wanasheria wakuu wa nchi  za Kenya,Rwanda na Uganda wamefunguliwa
mashitaka katika Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na
kukiuka vifungu vya Mkataba wa jumuiya hiyo.

Thursday, November 14, 2013

MKUTANO WAKUONYESHA MAHUSIANO YA KIJAMII KATI YA MAKAMPUNI YAFANYWA NA DARASA LA TARANGIRE KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA!!


Katika kujifunza kwa vitendo  somo la uhusiano wa kijamii wanafunzi  wa  darasa la Tarangire katika chuo  cha uandishi  wa habari na utangazaji  Arusha  wamefanya mkutano ulioonyesha mahusiano  kati ya kampuni na jamii.

Mmoja wa wanafunzi  wa darasa hilo Bi.Mgreth  Chigogwe alisema lengo la mkutano huo ni kuongeza uzoefu kwa wanafunzi waliosoma somo hilo ili kupata uelewa mpana katika taaluma hiyo ili watakapofuzu waweze kufanya kazi kwa ufanisi .

 Hata hivyo mmoja wa wakufunzi katika chuo hicho Bi.Prisca Mnzava   amesema kuwa kufanya mazoezi kwa vitendo  ni moja ya njia  ya kumjenga mwanafunzi katika msingi imara pindi wawapo chuoni.

Naye  Bw.Elifuraha Samboto ambaye  pia ni Mkufunzi  alitoa  wito kwa wanafunzi wanaosoma somo hilo waendelee kutia mkazo katika mazoezi  ya vitendo kwani ni njia ya mafanikio katika tasnia ya habari.

FUATILIA PICHA:
Mwanafunzi Mtaita Elieth aliyesimama kwenye nafasi ya Afisa mahusianoo wa kampuni akitoa maelezo mbalimbali kuhusu bidhaa inayozalishwa na kampuni yao waliyoitambulisha kwa jina la TARANGIRE.
 Mwanafunzi Gervas Danieli aliyesimama kwenye nafasi ya Mkurugenzi wa kampuni akitoa maelezo mbalimbali kuhusu bi kampuni yake waliyoitambulisha kwa jina la TARANGIRE.