NICE MEDIA WORKS

KWA WAIMBAJI WA INJILI

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, September 10, 2014


WAJASIRIAMALI WADOGO KATIKA SOKO LA KWA MROMBO WAMELALAMIKIA UONGOZI WA SOKO HILO KUTOKANA MFUMUKO WA BEI.









(Kutoka kushoto ni mjariliamali MAMA ABDULY akizungumza na na mwaandishi wa habari mapema jana)

Mmoja wa wa mfanya biashara katika soko hilo aliyejulikana kama ,MAMA ABDULY akizungumza na waandishi wa habari hapo jana  katika sokoni hapo nakusema kupanda kwa bei za nyanya pamoja na mboga ni changamoto kwao kwani wanashindwa kukidhi mahitaji yao pamoja na familia zao

Alisema kuwa wamekuwa wakinunua sanduku (tenga) moja kwa bei ya shilingi eilfu tisa(9000) mpaka eilfu ishirini na mbili(22000) lakini kwa sasa wananunua kwa shilingi (25000) mpaka sh.30000 kwa bei ambayo inaleta changamoto wakati wakuwauzia wateja wao kwani wanashindwa kuelewana.

"Mteja aliyezoea kununua nyanya kwa bei nafuu alafu anakuta bei imepanda  mpaka kumuelewesha inachukua mda kwa sababu anakuta nyanya za mia tano ni nne(4) na amezoea kwa kukuta ni nyanya sita au saba anashindwa kuelewa" alisema mama abduly.

Aidha mjasiriamali huyo aliweza kuzungumzia biashara nyingine ya mboga  kwani wakulima walikuwa wanawauzia mboga fungu moja sh.100 lakin sasa wanawauzia fungu 3 kwa shilingi mia tano.(500) bei ambayo ni kikwazo kwao.

"kama unavyoona sijasoma sana na nimeamua kujishughulisha na biashara hii ya uuzaji wa nyanya na mbogamboga kwa kukidhi mahitaji yangu       pamoja na familia yangu pia nasomesha watoto kupitia biashara hii,nimenunua kiwanja kupitia biashara hii ambapo ni faida nayoipata lakini sasa nashindwa  kupta faida kutokana na bei hizikabisa",alisema

Pamoja na hayo wafanya biashara hao wameendelea kusema kuwa 
changamoto hizo zinaambatana nakutokuwepo kwa choo,maji kwani ni huduma muhimi sanak wa jamii pamoja na sehemu maalum ya kufanyia biashara hizo kwani eneo hilo ambalo ni wanalitumia kwa sasa limekuwa dogo kutokana kuwa na wafanya biasharakatika eneo hilo.

Pia wafanya biashara hao walimazia kwa kusema wanauomba uongozi wa soko hilo kuwatengea eneo maalum kwa ajili ya biashara hiyo kwani eneo hilo wnaolifanyia biashara ni changamoto kwao na dogo sana kwani eneo hilo liko kandokandona barabara ikiwa nia hatari kwa maisha yao..HABARI NA ELIZABETH NJAU,PICHA NA GEORGE HILONGA



Tuesday, September 9, 2014

WANAFUZI WA AJTC WAASWA KUWA NA MWITIKIO KWENYE MASHINDANO YA UTANGZAJI

Mkuu wa idara ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaziji arusha bwana Onesmo Elia Mbise akifanya  maojiano na mwanishi wetu (picha na mwanaidi omary)


Mkuu wa idara ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaziji arusha bwana Onesmo Elia Mbise amewaasa wanafunzi wa chuo hicho kuwa na mwitukio pindi yanapotokea katika mashindano ya utangazaji
Amesema dhumuni la mashindano hayo ni kuinua vipaji vya utangazaji  na kuimarisha wanafunzi katika uandaji wa vipindi wa radio na Tv

Monday, September 1, 2014

ujerumani kuwapatia sila wakurd


Ujerumani inatarajia kulitumia jeshi la Wakurd wa Iraq silaha ikiwemo bunduki na silaha zile zenye mfumo unaoweza kukabiliana na mashambulizi ya vifaru vya kivita.
Jeshi hilo limekuwa likipambana na wapiganaji wa kiislamu kaskazini mwa Iraq.

Amesema uamuzi huo ni kutokana na maslahi ya nchi yake.Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula Von der Leyen amesema silaha hizo zotaweza kuwatosheleza wanajeshi elfu nne ifikapo mwishoni mwa Septemba.
Hatua hiyo iliyochukuliwa na Ujerumani imeelezwa kuwa ni ya nadra sana kwa nchi hiyo, kupeleka silaha kwenye eneo lenye mapigano.
Hata hivyo uamuzi huo umekosolewa na baadhi ya watu ambao wana wasiwasi zitakapoishia silaha hizo.                                                                                                 na mwandishi wako kennedy rutta

TULIPOFIKIA TUSIRUHUSU TENA SIASA IENDESHE UCHUMI =



 Katika utawala wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa na uchumi huria, kuendeleza mfumo uleule wa kizamani katika medani ya siasa, mathalan, dhana ya “chama tawala”; “chama kushika hatamu za uongozi”; “chama kimoja”; “zidumu fikra za mwenyekiti”, kwa moyo wa dhati kabisa, lazima niseme kwamba, kwa mtindo huo, Watanzania tutajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe.


Mabadiliko au mageuzi ya kiuchumi tuliyoyatarajia hayatakuwepo asilani . Nchi za wenzetu duniani, na hata za majirani zetu, zitasonga mbele kiuchumi, tena kwa kasi, lakini sisi tutabakia hapa tulipo, na pengine tukarudi nyuma zaidi kimaendeleo.

Kwa sababu, sisi tutakaposinzia, tutawapa mwanya wenzetu wa nje waje zaidi kuwekeza nchini. Wachote zaidi kilichopatikana, na kukipeleka kwao, wakituacha na umaskini wetu.

Tumekiona hicho kikifanyika katika sekta ya madini na rasilimali nyingine za nchi, ambazo Watanzania wenyewe hawakuwa na ubavu wa kuwekeza vilivyo.
Ukweli ni kwamba Watanzania tutaendelea kujikongoja kwa mwendo wa Konokono, tukiomba Mungu tusipishane na gari yanayoendeshwa na wawekezaji kutoka nje wenye mitaji mikubwa’.

Watanzania tutabakia tumenasa, na hata ikibidi kuzama zaidi katika lindi la ufukara na umaskini .

Watu hawatakuwa na uwezo wa kuwekeza na kuendesha miradi mikubwa ya kiuchumi yenye uwezo wa kuleta mabadiliko makubwa haraka (BRN), kama wengi walivyotarajia

Kwa nini ? Kwa sababu tutakuwa tumekubali kuruhusu ushindani katika uchumi, yaani nguvu za soko na sekta binafsi ziongoze uchumi na biashara.
Lakini, bado tutakuwa wagumu au tumeshikwa na kigugumizi katika kuruhusu ushindani wa kweli katika medani ya siasa kwa kuruhusu au kukubali kuwa na Katiba mpya itakayoruhusu na kufungua milango ya ushindani wa kisiasa, na Katiba hiyo mpya kuwa mhimili wa kweli wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, kwa kutengeneza uwanja ulio sawa wa ushindani wa kisiasa, miongoni mwa vyama vya siasa nchini, bila kuruhusu ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Wenzetu wamepiga hatua kubwa kiuchumi kwa sababu ya ubora na umakini wa katiba zao. Katiba zao zimejenga ushindani wa kisiasa uliokidhi mahitaji ya ushindani wa kiuchumi .

Kwa kuwa tumekubali ushindani wa kiuchumi, hatuna budi kukubali ushindani wa kweli na wa haki kisiasa. Vitu hivyo viwili daima huenda pamoja, vikiachana lazima patatokea mtafaruku kimaendeleo.

Ziko wapi tena nguvu za umma katika vyama vya siasa, wakati mashirika yao ya umma yaliuawa na wajanja wachache na wao wakaachwa yatima ?
Ziko wapi tena zama za nguvu ya umma, kwa kutoa ahadi za nafasi nyingi zaidi za ajira, na hali bora zaidi ya maisha, wakati viwanda vyao vilipukutika na kubakia maghofu na nchi kugeuzwa dampo la bidhaa duni kutoka nje?
Wakati migodi yote muhimu ikimilikishwa kwa wageni (kampuni za kimataifa), na wao wakibakia na vumbi lisilo na utajiri wa uhakika?
Katika mazingira kama hayo ya uchumi shindani, bila ya kuruhusu siasa shindani itakayoongoza na kulindwa na Katiba mpya na bora, iliyobeba maudhui hayo ya mageuzi ya kiuchumi, basi tujue kwa hakika kwamba Watanzania tutajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe.

Hakuna cha maana kitakachofanyika kiuchumi katika dunia hii ya utandawazi. Utegemezi wa kiuchumi na kiteknolojia utazidi kuongezeka kwa kukosa ubunifu wa kifikra na mawazo mbadala.

habari  na   winlady   johaness  mbesere

Mlipuko waua a mjini Paris.

na GIFT ADISON

Jengo lililolipuliwa

Mlipuko umeharibu jengo moja la ghorofa 4 kazkazini mashariki mwa Paris na kumuua mvulana mmoja huku watu kadhaa wakiwa hawajulikani walipo.
Watano kati ya wale waliotoweka wanadaiwa kuwa watoto.
Afisa mmoja wa huduma ya zima moto katika mji huo mkuu amesema haijulikani ni nini kilichosababisha mlipuko huo.
Msemaji huyo amesema kuwa maafisa wa matibabu wamepelekwa katika eneo hilo.

Putin aelekeza shutuma Ukraine Mashariki


habari EVALIYNE BAKARI
Mwanaharakati wa demokrasi aliyetuhumiwa na wapiganaji kuwa jasusi wa serikali ya Ukraine, apigwa teke na mpita njia na kuzomewa mjini Donetsk
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametoa wito kufanywe mazungumzo ya haraka kuhusu uhuru wa mashariki mwa Ukraine, kama sehemu ya mazungumzo ya kumaliza vita vya huko.
Bwana Putin amenukuliwa akisema kuwa "masilahi ya haki" ya watu wanaoishi katika jimbo hilo lazima yalindwe.
Mwandishi wa BBC anasema matamshi ya Rais Putin ni ishara kuwa Urusi inataka serikali ya Ukraine izungumze moja kwa moja na wapiganaji wanaoipendelea Urusi, kuhusu amani.
Urusi ina hamu ya kuongoza mchakato huo.
Rais Putin amesema hayo siku moja kabla ya mazungumzo kuanza mjini Minsk, Belarus ( nchi jirani na Ukraine) baina ya Ukraine, Urusi na Umoja wa Ulaya, kujadili msukosuko huo.
Na Umoja wa Ulaya na serikali ya Ukraine wameonya kuwa hali katika eneo hilo inakaribia kufika kiwango ambapo hali ya zamani haitoweza kurejeshwa tena.
Na katika tukio jengine Ukraine imekabidhi askari 10 wa miamvuli kwa Urusi, na Urusi imewarejesha wanajeshi 63 wa Ukraine.

VIKOSI VYA USALAMA VYAPAMBANA NA AL-SHABAB SOMALIA..

Vikosi vya usalama vya Somalia vimezima shambulio la wanamgambo wa al Shabab katika makao makuu ya masuala ya kiintelijinsia na kitengo cha mahabusu huko Mogadishu mji mkuu wa nchi hiyo.

 Polisi na watu walioshuhudia wameeleza kuwa shambulio hilo la leo lilianza baada ya kulipuka gari lililokuwa limetegwa bomu nje ya kituo cha taifa cha masuala ya intelijinsia, mlipuko uliofuatiwa na shambulio la watu wenye silaha waliovalia sare za jeshi la taifa la Somalia.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Somalia amesema kuwa mmoja wa wavamizi ameuawa kwenye mlipuko wa bomu na wengine sita wameuliwa na vikosi vya usalama.  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Somalia ameongeza kuwa shambulio hilo limekwisha na kwamba wavamizi wameshindwa kutimiza lengo lao la kuvuruga oparesheni ya bahari ya Hindi akiashiria oparesheni ya nchi kavu inayotekelezwa sasa na Umoja wa Afrika na serikali ya Somalia. Wakati huo huo Msemaji wa kundi la al Shabab Abdulaziz Abu Musab amethitibitisha shambulio hilo na kudai kuwa wanamgambo wao wamewaua maafisa kumi wa usalama na kuwaachia huru mahabusu kadhaa.



Habari na Theodora Massawe
Chanzo:BBC