NICE MEDIA WORKS

KWA WAIMBAJI WA INJILI

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, July 3, 2014

Ridhiwani Kikwete amudu kikaango

Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhwani Kikwete leo hii imekuwa ni zamu yake kushiriki kuchat Live na wananchi pamoja na wafuasi wake kupitia Kikaangoni Live ya ukurasa wa Facebook wa EATV, ambao unahusisha familia kubwa kabisa ya mashabiki.

Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete, kupitia ukurasa wetu wa Facebook ameweza kuelezea mambo mbalimbali yanayomhusu wakati akijibu maswali ya mashabiki wake katika ulingo wa siasa na kama mtoto wa Rais.

Ridhiwani amekiri kupata maswali mengi ambayo yamekuwa changamoto kwake ambapo yamemlenga kwa namna moja au nyingine kuhusiana na ulingo wa siasa na pia hakuacha kutoa pongezi zake kwa msanii Diamond ambaye aliiwakilisha nchi alipokuwa "nominated" katika tuzo za BET zilizofanyika hivi majuzi nchini Marekani.

Zoezi hili linafanyika kila Jumatano saa 6 mpaka saa 8 mchana kupitia www.facebook.com/eatv.tv, Like ukurasa huu kama bado hujafanya hivyo ili kuwa sehemu ya familia hii kubwa, na kaa tayari kwa staa mwingine mkali kupitia Kikaangoni Live wiki ijayo.

Wavulana 19 wameaga dunia mwaka huu katika sherehe za kuwapasha tohara wavulana

Wizara ya Afya nchini Afrika Kusini inasema kuwa wavulana kumi na tisa wameaga dunia mwaka huu katika sherehe za kitamaduni za kuwapasha tohara wavulana.

Tohara hiyo ni utamaduni unaopewa heshima kubwa katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo.

Utamaduni wa tohara ni muhimu kwa vijana hasa kwa kuwa ni njia ya vijana kuingia utu uzima, lakini baadhi hufariki wakipitia utamaduni huo na wengine hupoteza sehemu zao nyeti.
Vijana 19 wamefariki kufika sasa na wengine 50 wako hospitalini.

Wanapokea matibabu ya kukosa maji mwilini, sehemu zao za siri kuoza na majerahe mengine mabaya.

Wazee wa kijamii wasiokuwa na mafunzo ya kufanya tohara ambao huendesha vituo vya kuwapasha tohara vijana wamelaumiwa kwa vifo kama hivyo.

Katika baadhi ya visa ambavyo vimeripotiwa, vijana hutoroka na kujiunga na vijana wengine wanaokwenda katika vituo hivyo haramu bila ya idhini ya wazazi.

Serikali imewasihi wazee wa kijamii kushirikiana na watu wenye uwezo wa kitaalamu na madaktari ili kuwapasha tohara vijana na kuzuia vifo.

Mwezi jana watu 23 walikamatwa kwa vifo vya vijana waliofariki kutokana na athari za kupashwa toihara.

Na Irene V Lymo.

Wednesday, July 2, 2014

BONANZA LA WANAHABARI ARUSHA LAFANA. PINTO AAHIDI KUSAIDIA KUBORESHA LIJALO

NA: NURU PAULO FERUZ

Arusha.Timu ya soka na ya mpira wa pete za Chuo Cha Uandishi wa Habari Arusha (AJTC) juzi zilitwaa ubingwa katika bonanza la tisa la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini.
Katika bonanza hilo, lilifanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kuandaliwa na Taswa Arusha na kampuni ya Ms Unique, jumla ya timu 10 zilishiriki kutoka mkoa wa Arusha na Manyara.
Timu ya soka ya AJTC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya Radio Sunrise, wakati wasichana wa timu hiyo, waliwashinda timu ya chuo cha  uandishi wa habari na maendeleo ya jamii (IMS), magoli 18-5.
Mgeni rasmi katika bonanza Mwenyekiti wa Taswa Taifa, Juma Pinto alikabidhi vikombe na fedha taslimu, ambapo bingwa wa very soka alipewa kikombe, ,fedha taslimu 200,000 na seti ya jezi.
Huku mshindi wa pili soka akipata 100, 000 wakati bingwa wa mpira wa pete alizawadiwa kikombe cha fedha taslimu 100, 000 huku mshindi wa pili akikabidhiwa tsh 50, 000.
Katika bonanza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia nchini, (Tbl), kampuni ya Megatrade Investment, Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, Cocacola, SBC (T) ltd, AICC, Tanzanite Forever, TANAPA na Alphatel timu nyingine zilizoshiriki ni Radio 5.
Nyingine ni timu ya Arusha One, ORS kutoka mkoa wa Manyara, Salam Club, IMS na  Taswa Arusha Arusha ambayo iliambulia ushindi katika kukamata kuku.
Akizungumza katika bonanza hilo, Pinto alipongeza washindi na viongozi wa Taswa Arusha kwa kazi the nzuri waliofanya.
Pinto pia aliahidi katika maadhimidho ya miaka 10 ya bonanza hilo, mkutano mkuu wa T aswa Taifa utafanyik a Arusha sambamba na tuzo za waandishi bora.
Awali Meneja matukio wa TBl, Chris Sarakana aliahidi Tbl kuendelea kudhamini bonanza hilo kutokana na kuvutia wanahabari na wakazi wengi wa Arusha.
Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway aliwapongeza wanahabari kwa kushiriki kwa wingi katika bonanza hilo na kuahidi kue kudhamini.

Tuesday, July 1, 2014

Je Urembo wa kujichubua ni urembo?


Picha za hivi karibuni za Vera Sidika kwenye mitandao ya kijamii
Swala la kubadili rangi ya ngozi limekuwa kama msumari moto, kunao wanaoliunga mkono na wale wanaolipinga swala hilo katu hawawezi kulifanya.

Baadhi wanasema kuwa ni wanawake wasiojithamini na kujiamini pekee ndio wenye kujichubua ngozi.

Mjadala huo ukiendelea, wasichana wengi wanajitafutia umaarufu sio Marekani na Uingereza tu bali hata katika kanda ya Afrika ya Mashariki. Wasichana hao wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kupata huo umaarufu.

Picha za awali kabla ya Vera kujichubua ngozi
Mmoja wa wasichana hao ni Vera Sidika anayejulikana sana nchini Kenya na Afrika mashariki kwa kuwa na makalio makubwa ambayo ndiyo yaliyompa umaarufu wake baada ya kuonekana katika wimbo mmoja wa video uitwao 'You Guy' ambao baadaye ulipigwa marufuku nchini Kenya.

Vera amejizidishia umaarufu kwa kubadili rangi yake ya ngozi, zamani kidogo akiwa mweusi na sasa amejichubua na kuwa mweupe na pia kuwaambia watu kuwa kubadili rangi ya ngozi yake ni yeye mwenyewe kujitakia. Hiyo isiwashughulishe watu.

Vera anajulikana kwa kuwa na mazoea ya kujipiga picha hasa za makalio yake na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii. Vara analinganishwa sana na Kim Kardhashian hasa kwa sababu ya umbo lake.

Kazi ya Vera hasa ni ya uwanamitido lakini mbali na hilo Vera hulipwa ili kufika kwenye karamu mbali mbali , kwenye disco na katika hafla mbali mbali za watu mashuhuri. Yeye pia hulipwa kuwa katika kanda za video za wanamuziki maarufu Afrika Mashariki.

Alifichua kupitia televisheni Ijumaa kuwa alitumia maelfu ya dola kubadili rangi ya ngozi yake na kujifanya mweupe.

Shughuli hiyo aliifanyia nchini Uingereza na ilimgharimu karibu milioni 15 pesa za Kenya, hizo ni dola 170,000 na kwamba tayari kuna watu wengi wanaotaka sana kujichubua ngozi na kufanana na Vera, kwa mujibu wa mwanadada huyo.

Vera ni mwanamitindo na anapanga kufungua duka la kuuzwa bidhaa za urembo
Vera anasema kuwa watu wamemsema sana kwenye mitandao ya kijamii vibaya kwa sababu ya anavyoendesha maisha yake.
Amewataja kama wanafiki kwa sababu anasema huku wakiendelea kumsema na kumkosoa kwa kujichubua, wamekuwa wakimuuliza alichofanya ili na wao watafute pesa wakafanye hivyo kwa wanataka sana kufanan naye.

Mtindo wa wanawake kujichubua ni swala tata nchini Kenya. Sio kama India ambako vipodozi vya kujichubua huuzwa wazi wazi. Nchini Kenya bidhaa hizo, huuzwa kimagendo.

Wataalamu wanasema, wanawake wengi wanaendelea kujichubua licha ya hatari za bidhaa zinazouzwa kimagendo.

Swala la wanawake kijichubua barani Afrika lilianza kujadiliwa waziwazi pale ambapo msanii raia wa Cameroon Dencia kuzindua rasmi bidhaa zake za kuchubua ngozi ziitwazo, Whitenicious.

AJTC WAIBUKA KIDEDEA KWENYE BONANZA LA WAANDISHI WA HABARI MKOANI ARUSHA

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo nchini(Taswa)Juma Pinto(kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa kudumu wa Taswa mkoa wa Arusha,Jamila Omary aka "Dangote" wakati wa Bonanza la vyombo vya lililopigwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mgeni Rasmi katika Bonanza la Vyombo vya Habari mkoani Arusha,Juma Pinto wa pili kushoto,akifatilia michezo iliyokua inaendelea kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wengine kushoto ni Le Mutuz,Mkurugenzi wa Gogobichi Media,Joseph Lyimo na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mega Trade,Goodluck Kway

Washindi wa kukimbiza Kuku  kutoka The Institute of Media and Social Studies(IMS) "wakishow"

Katibu wa Kudumu wa Taswa Arusha,Mussa Juma(shoto) akiwa Le Mutuz baada ya kukagua timu za Arusha One Radio na Arusha Journalism Training College(AJTC)

Mabingwa katika mpira wa miguu na mpira wa Pete(Netball)Chuo cha Arusha Journalism Training College(AJTC)wakishangilia ushindi wao.

Waandishi wa habari za michezo wakifatilia burudani.

WAKUFUNZI wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakifuatilia mwenendo wa Mchezo kati ya Sunrise Redio na  Chuo cha  hicho cha AJTC

 
Baathi ya wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakifuatilia kwa makini Mpambano.


Katibu Msaidizi wa Taswa Arusha na Mtangazaji Mahiri wa vipindi vya Michezo na Burudani,Hamza Kalemera akichapa kazi,kulia ni Mussa Juma

Friday, June 6, 2014

TBL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA USAFI WA MAZINGIRA VYA SH MIL 15 MANISPAA YA ILALA

 Meneja wa Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL), Emma Oriyo (kushoto) akishiriki na viongozi mbalimbali kufanya usafi, Ilala, Dar es Salaam juzi, katika  maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Dar es Salaa
 Meneja wa Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL), Emma Oriyo (kushoto) akishiriki na viongozi mbalimbali kufanya usafi, Ilala, Dar es Salaam juzi, katika  maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Dar es Salaam.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa,(wa pili kulia) akishiriki na viongozi mbalimbali  na wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kufanya usafi Ilala, Dar es Salaam, katika  maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akikabidhiwa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.mil. 15 na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu katika hafla iliyofanyika, Ilala, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani. Wafanyakazi wa TBL walishiriki kufanya usafi eneo la Karume, Ilala. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa TBL, Emma Oriyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati)akikabidhiwa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.mil. 15 na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu katika  hafla iliyofanyika, Ilala, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani. Wafanyakazi wa TBL walishiriki kufanya usafi eneo la Karume, Ilala. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa TBL, Emma Oriyo.

TUKIO KATIKA PICHA: MAMIA YA WATU WAJITOKEZA KUMSINDIKIZA MTOTO NARSA(MTOTO WA KWENYE BOKSI) KATIKA UWANJA WA JAMHURI MOROGORO

 Umati wa watu uliofurika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kuaga mwili wa Nasra.
Wanafunzi wa Shule za Msingi Mkoani Morogoro nao walijumuika kumuaga mtoto Nasra Rashid katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro                      


na neema mushi