NICE MEDIA WORKS

KWA WAIMBAJI WA INJILI

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, June 6, 2014

HABARI PICHA ZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA NJOMBE

 

  


 Deo Sanga ambaye ni Mbunge na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe.


Aliyekuwa  mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe, Adam Ismail Msigwa (pichani) ambaye alijukana kwa jina maarufu kama 'Shilingi ni Vita' amefariki  nyumbani katika Mitaa wa Kwivaha Njombe mjini na mazishi yalifanyika katika kijiji cha lisitu.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Cept. mstaafu Aseri Msangi (kushoto ) wa pili ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw Saitabau na wa mwisho (kulia) ni Kamanda wa polisi mkoa  SACP  Ngonyani.
"MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI"
 'AMINA
Na janeth mbunito

TAHA KUSHIRIKIANA NA SIDO WAANDAA MONYESHO YA WAJASIRIAMALI WADOGO WADOGO




 meneja wa shirika la SIDO  Isdori  Kiyenze Akiwa anaongelea maonyesho hayo jinsi yatakavyokuwepo ambapo alisema zaidi ya wafanyabiashara wadogo wadogo 250 watashiriki


Mkurugenzi wa TAHA, Bi Jacqueline Mkindi akiwa anawaelezea waandishi wa habari nia haswa ya wao kama taha kushiriki kuandaa maonyesho haya

 waandhishi wa habari wakiwa   kikazi zaidi

Tanzania Tanzania Horticultural Association (TAHA)  kwa kushirikiana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) wameandaa maonyesho ya siku sita kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi pamoja na wajasiriamali jinsi ya kuzifanya bidhaa zao kuwa na ubora wa kimataifa.

Akiongea leo na waandishi wa habari meneja wa shirika la SIDO  Isdori  Kiyenze alisema  kuwa maonyesho hayo yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe saba  hadi kumi na mbili ambapo alibainisha kuwa yanatarajiwa kufunguliwa june 9 na waziri wa viwanda na biashara Abudala kigoda katika viwanja vya makumbusho vilivyopo jijini hapa.

Alisema kuwa nia haswa ya kuandaa maonyesho haya  nikuwajengea uwezo mkubwa wajasiriamali wadogo wadogo na kuwafundisha namna  mbalimbali za kisasa za kutengeneza bidhaa zao na kuzihifadhi (kuparki) katika hali nzuri ya kimataifa ikiwa ni pamoja na kusindika .

Alisema kuwa pia watatoa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafundisha teknoligia  mbalimbali za kisasa zinazofanya kazi katika kipindi hichi.

“unajua  wajasirimali wetu wengi wamekuwa wanatengeneza vitu  vizuri na vyenye ubora ambavyo avina tofauti na vya nchi zingine  lakini vimekuwa avithaminiwi sasa sisi kama sido tumepita katika supermarket mbalimbali tumeangalia vitu vilivyosindikwa tukaona sasa havina tofauti na vitu vyetu ambavyo tunalima tukaamua kuwapa elimu wajasirimali wetu sasa kunawengine ambao hawakupata elimu ndo tunataka tuwape katika kipindi hichi cha maonyesho haya”alisema Kiyenze

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TAHA, Bi Jacqueline Mkindi alisema kuwa  wao kama taha wameamua kushirikiana na sido kuandaa maonyesho haya ili kuweza kuwajengea uwezo zaidi wajasirimali wadogowadogo .

Alisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakiweka nguvu zao  nyingi kwa wazalishaji lakini kwa sasa wameamua kungia na huku ili kuweza kuwasaidia wafanyabiashara hawa wadogo wadogo kusogea mbale zaidi na kuelimika ambapo wakielimika  kutakuwepo na  ongezeko la dhamani.

Aidha wamesema kuwa kwa sasa ivi wameamaa kuwatafuta na kufanya kazi nao ili kuweza kuwasaidia kutangaza bidhaa zao ambazo zinatengenezwa hapa nyumbani.
 
NA JANETH KIWALE

MBOWE AANZA ZIARANI HAI JIMBONI KWAKE


 Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akishuhudia uharibifu kwenye moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Weruweru iliyoko wilayani Hai, ikiwa ni sehemu ya ziara yake anayofanya pamoja na kamati yake ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF), kwa ajili ya kutathmini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake ili mfuko huo uweze kusaidia kuongeza nguvu za ujenzi. Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mfuko huo alielezwa kuwa shimo hilo limekuwa likitumika na wananchi waovu kama 'mlango' wa kuingia na kutoka kwa ajili ya kuiba kuni zinazotunzwa katika chumba hicho cha darasa.

Mmoja wa Wanakamati wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo (CDF) Jimbo la Hai akipanga kuni katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Shirimatunda iliyoko wilayani Hai, wakati Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Freeman Mbowe (Mbunge wa Hai), alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambayo mfuko huo utasaidia kuongeza nguvu za ujenzi. Chumba hicho mbali ya kutumika na wanafunzi kwa ajili ya kusomea, pia kinatumika kama stoo ya kuni za kupikia chakula cha wanafunzi shuleni hapo, hali ambayo inadhihirisha kuwepo kwa mahitaji ya vyumba kwa ajili ya matumizi mbalimbali.  
 
NA GAUDENSIA NGETI

MTOTO WA MAREHEMU TYSON "SONIA" ATOA WOSIA MZITO KUHUSU KIFO CHA BABA YAKE, SIKILIZA SAUTI YAKE HAPA

Juzi  simanzi ma majonzi vilitawala katika viwanja vya Leaders Club wakati mamia ya watu walipokuwa wakiaga mwili wa muongozaji wa filamu na vipindi vya televisheni, George Tyson aliyefariki katika ajali ya gari.
 
Moja kati ya matukio yaliyowatoa machozi mamia ya watu waliohudhuria katika tukio la kumuaga Tyson, ni pale mtoto wake wa kike aitwae Sonia alipokuwa akitoa neno/ujumbe wa kumuaga baba yake.
 
Sonia aliongea kwa majonzi maneno yaliyosababisha watu wengi watokwe machozi.
 
“You were kind na rafiki yangu kipenzi. Ulikuwa mtu ambaye ni rahisi kuongea nae na kunielewa. Daima ulikuwa unanitunza na kunidekeza. Na mara ya mwisho kuonana na wewe wiki iliyopita ulinambia ni jinsi gani nimekufanya uwe pride na mimi. And moreover I sing…I take a breath away. Na ninakuahidi, sitaacha kuimba kwa ajili yako. Nataka ufahamu kwamba nitakupenda milele. I will always Love You dad. Rest In Peace.”
 
Sonia ni mtoto wa marehemu aliyempata na muigizaji Monalisa ambaye pia ni mtangazaji wa 100.5 Times Fm.
 
credit: eddy blog
Na Flaviana makawia 

Tajiri adaiwa kumng’ata, kumchoma pasi mtumishi wake kwa miaka mitatu


  Yusta Lucas akionyesha makovu yake ya mgongoni ambayo aliyapata kwa kung'atwa na kuchomwa na pasi na mwajili wake. Picha na Esther Kabakay


Dar es Salaam. Mfanyakazi wa ndani, Yusta Lucas (20) amekumbana na masahibu yanayofanana na yale ya mtoto Nasra Mvungi (4) aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka karibu minne huko Morogoro. Huyu amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam akiuguza majeraha yanayotokana na kuteswa na kufungiwa ndani kwa miaka mitatu.
Binti huyo, mwenyeji wa Mkoa wa Tabora, katika Kijiji cha Kampala amedai kuwa amekuwa akiteswa na kufungiwa ndani ya nyumba na tajiri yake, Amina Maige wa Mwananyamala, Kwa Manjunju katika kipindi chote hicho. Amina anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba OB/RB/9967/2014.
Akisimulia masahibu yaliyompata akiwa katika Wodi Namba Tatu ya hospitali hiyo, Yusta alisema: “Nililetwa Dar es Salaam mwaka 2010 kufanya kazi za nyumbani baada ya bosi wangu (Amina) ambaye ni binamu yangu kuzungumza na mama yangu na kuniomba nije kumsaidia kazi ndogondogo.”
Alisema aliishi vizuri na mwajiri wake huyo, lakini mwaka 2012 ndipo mambo yalipoanza kubadilika akidai kuwa Amina alianza kumwadhibu kwa kumng’ata na kumchoma kwa pasi kila alipomtuhumu kutokufanya kazi zake vizuri.
“Alikuwa akinichapa na kuning’ata sehemu mbalimbali wakati mwingine usoni, pia kunichoma kwa pasi yenye moto kila aliponituhumu kutokufagia au kupiga deki vizuri.”
Hakuwahi kupelekwa hospitali
Alisema licha ya kupata vidonda kutokana na adhabu hizo, mwajiri wake huyo hakuwahi kumpeleka hospitali na pale alipoona hali ni mbaya alimnunulia dawa... “Tunaishi wawili tu baada ya kuondoka mumewe na mtoto wake kumpeleka shule ya bweni... niliugulia hadi nikapona bila mtu mwingine kufahamu.”
“Akienda kazini anafunga geti na kunikataza kufungua hata kama mtu atagonga… sokoni nilikuwa naenda siku ambazo yeye yupo tu na huwa akiniamrisha niende haraka na kurudi pasipo kuzungumza na mtu yeyote.”
Alisema mwajiri wake huyo alikuwa akituma pesa za mshahara wake kwa mama yake akisema ndiye anayepaswa kulipwa, jambo ambalo anadhani limemfanya mama yake kuhisi mwanaye yuko katika mikono salama... “Kila alipotuma alipiga simu na kunipa niongee na mama kuhakikisha kama zimefika huku akinisimamia na baada ya hapo anachukua simu.”
Ataka kurudi kwao
Binti huyo ambaye sehemu kubwa ya mwili wake ina alama za kung’atwa meno na majeraha ya kuchomwa na pasi, alisema: “Ninaomba mtu yeyote mwenye hela, nataka nikitoka hapa hospitali nirudi Tabora kwa mama. Nina shaka na maisha yangu hapa kwa huyu mama… sitaki tena kubaki Dar es Salaam kutokana na mateso ninayoyapata.

credit: mwananchi
Na Dorcas Mdemu

Warioba azishukia Ukawa, CCM kuepusha migogoro isiyo na tija



 

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewashauri wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na CCM kuacha kuzunguka mikoani kufanya mikutano inayoeleza misimamo yao kuhusu mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa haina tija kwa taifa.
Ameonya kuwa mikutano hiyo inajenga mwelekeo mbaya kwa taifa na kuhatarisha mchakato wa Katiba na kuzitaka pande hizo kumaliza tofauti zao.
Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika Dar es Salaam jana, Warioba alisema: “Kwa mustakabali mwema wa taifa, ni muhimu makundi haya ‘ya-resolve’ (yamalize), matatizo yaliyopo kabla ya Agosti, ili Bunge Maalumu la Katiba likirejea, wote washiriki na kukamilisha mchakato wa kupata Katiba Mpya. Hili ni kwa masilahi ya taifa.”
Kauli ya Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu, imekuja huku makundi ya Ukawa linaloundwa na wabunge wengi wa upinzani na viongozi wa CCM wakiendelea kung’ang’ania misimamo yao kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Wakati CCM ikipinga mapendekezo ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu uliomo kwenye Rasimu, Ukawa unaunga mkono mapendekezo hayo.
Aprili 16, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliiongoza Ukawa kutoka ndani ya Bunge la Katiba baada ya kumaliza kuchangia mjadala huo, kwa madai ya kutokutendewa haki na CCM katika mambo mbalimbali ikiwamo kupinga mapendekezo ya upinzani hata yale ya msingi akisema hawawezi kuwa sehemu ya watu wanaosambaza chuki na kuwa sehemu ya kuibomoa nchi.
Siku chache baadaye, Ukawa ulianza mikutano nchi nzima kwa kile ulichodai kuwaeleza wananchi namna CCM inavyotaka kuchakachua maoni yao yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Kwa upande wake, CCM imekuwa ikifanya mikutano kueleza msimamo na sababu za kutaka kuendelea kwa muundo wa serikali mbili.
Jaji Warioba alisema makundi hayo yana nafasi ya kumaliza tofauti zao kabla ya Bunge Maalumu la Katiba kuanza tena vikao vyake, hivyo kuliwezesha taifa kupata Katiba Mpya.
Alisema makundi hayo yasipopatana yanaweza kuhatarisha mustakabali wa taifa hata amani iliyopo.
Alionya kuwa amani iliyopo nchini ikivurugika kwa sababu yoyote ni vigumu kuirejesha na kwamba watakaotaabika ni wananchi.
Jaji Warioba ambaye aliwahi kuongoza Tume ya Rushwa iliyoundwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, alisema amani ya Tanzania ikivurugika kutokana na makundi kupingana katika mchakato wa Katiba wanasiasa ndio watakaonyooshewa vidole.
 credit: Mwananchi
Augustina kawau.

MAXIMO ATAJA WASAIDIZI WAKE, NI WATANZANIA


KOCHA Marcio Maximo kutoka Brazil, tayari ameupitia mkataba wa kuanza kufanya kazi Yanga na kusema: “Nitaanza kazi na (Charles) Mkwasa pamoja na (Juma) Pondamali.”
Awali kulikuwa na hofu huenda kocha huyo angetaka kutua nchini na msaidizi wake kutoka Brazil lakini sasa atalazimika kuwataja wazawa hao katika benchi lake la ufundi.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinaeleza Maximo ametumiwa mkataba huo ambao awali ulipitiwa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji na ukatumwa nchini Brazil kupitia mwakilishi wake anayeishi jijini Dar es Salaam na amekubali kushirikiana na Mkwasa na Pondamali.
Suala la kocha msaidizi kutoka Brazil, Yanga na Maximo walikubaliana kuwa, atakapokaa mwaka mmoja na kufanya kazi kwa mafanikio, basi Yanga inaweza kuliangalia hilo kama wamuongeze kwenye benchi la ufundi.
Mwakilishi huyo wa Maximo ambaye amekuwa akisimamia zoezi hilo, ameutuma mkataba huo na Maximo ameupokea na kuupitia.
Habari za uhakika zinaeleza, inachotaka Yanga ni Maximo kupunguza dau lake ambalo alianzia dola 16,000 (zaidi ya shilingi milioni 25) kwa mwezi kabla ya kushuka hadi dola 15,000 (zaidi ya shilingi milioni 24), lakini Yanga imesisitiza inataka ashuke kidogo.
Ahadi nyingine ambazo amepewa Maximo ni nyumba na gari la kutumia pamoja na marupurupu mengine ambayo hayajajulikana.
Championi kama kawaida, ndiyo lilikuwa ni gazeti la kwanza kuandika kuhusiana na ujio wa Maximo, taarifa hiyo ilitoka wiki nne zilizopita.
Iwapo Maximo ataupitia mkataba huo na kuukubali, atatua nchini ndani ya siku nne zijazo na kusaini mkataba huo kabla ya kuanza kazi moja kwa moja.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji alisema mbele ya wanachama kwamba yuko katika hatua za mwisho kuhakikisha Maximo anatua nchini.
Maximo atafanya kazi na makocha wazalendo, Charles Boniface Mkwasa na Juma Pondamali na huo ndiyo umekuwa msimamo wa Manji.
Pondamali aliwahi kufanya kazi na Maximo wakati akiwa katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Katika majadiliano yanayoendelea kati ya Yanga na Maximo ni pamoja na suala la kipa Juma Kaseja ambaye hakuwa na uhusiano mzuri na kocha huyo wakati akiinoa Stars.
Maximo akimalizana na Yanga na kuanza kazi, rasmi atakuwa amechukua nafasi ya Hans van der Pluijm anayekwenda kupiga kazi nchini Saudi Arabia ambaye pia alichukua nafasi ya Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts.
NA ABRAHAM WILLIAM