NICE MEDIA WORKS

KWA WAIMBAJI WA INJILI

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, February 14, 2014

Ukimwi kwa vichanga; changamoto kubwa kwa jamii

 Na Mwajuma Abdul

Mamia ya wanawake nchini wapo katika huduma ya kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Ni mapema asubuhi katika kibaraza cha Hospitali ya Wilaya ya Tanga iliyoko Ngamiani, makumi ya kinamama wajawazito wameanza kuchukua nafasi katika benchi la kuingia katika chumba cha ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya Ukimwi (VVU) kabla ya kuendelea na huduma nyingine za uzazi.
Kinamama hao ni tofauti na wengine ambao wameishafanya kipimo hicho ambao wamefika hapo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya hali zao na kadri muda unavyokwenda ndivyo idadi inaongezeka kila mmoja akiwa ametoka umbali wake ili kuifikia huduma ya kliniki.

Lowassa, Sumaye, Ngeleja wajieleza Kamati ya Mangula



     Na Mariam George

          
 Mawaziri wakuu wa zamani, Frederick Sumaye (kulia) na Edward Lowassa wakizungumza Mjini Dodoma jana kabla ya kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM. Picha na Adam Mzee  

.Waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu; Edward Lowassa na Frederick Sumaye jana walifika mbele ya Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM kutoa maelezo juu ya tuhuma za kufanya kampeni za urais kabla ya wakati.
Mbali na wastaafu hao, mwingine ambaye jana alifika mbele ya kamati hiyo ambayo ilikuwa chini ya
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman
 Kinana ni Waziri wa Nishati wa zamani na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Mgomo wa EFD waisha

Na Mariam George
 
]Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa jumuiya za wafanyabiashara wa kati wa Kariakoo na mikoani kuhusu mgogoro wa matumizi ya mashine za kielektroniki za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jijini Dar es salaam, juzi. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu  

 Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) imetangaza kusitisha mgomo wa wafanyabiashara uliodumu kwa takriban siku tano kupinga notisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kuwapa siku 14 za kufunga Mashine za Elektroniki za Kutoza Kodi (EFD).

Mvua yaua,watu 300 hawana makazi

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatius Makunga.

Mtu mmoja amefariki na wengine zaidi ya 300 hawana mahali pa kuishi katika Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kubomoa nyumba zao.
 

Mbali na hasara hiyo, mvua hizo iliyonyesha kwa takribani siku nne sasa, pia zimeharibu vibaya zaidi ya ekari 60 za mazao ya chakula.
Familia hizo kwa sasa zinaishi kwa kutegemea hisani kutoka kwa wasamaria wema.

 

Habari zilizopatikana jana na baadaye kuthibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatius Makunga, zilileza kuwa tayari serikali kupitia Ofisi
ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa, kimetoa msaada wa chakula tani 1.5 kwa ajili ya kuhudumia waathirika wa tukio hilo.

Monday, February 3, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA MKOANI KILIMANJARO



Leo ni Law Day, tunamsubiri mgeni Rasmi
Wanasheria wakimsubiri Mgeni Rasmi
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi, Jaji Aisha Nyeyere, akiongoza Wanasheria katika maadhimisho ya siku ya Sheria (Law Day), yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mahakama Kuu kanda ya Moshi.

ONA WANAFUNZI WA ST. ANNE MARIE BONGO WALIVYOHARIBU MALI ZA SHULE YAO ONA HAPA LIVE!!

 Mkuu wa Wilaya ya Kinoniondoni, Jordan Rugimbana akikagua chumba cha kompyuta ambacho kumefanyika uharibifu mkubwa na kuharibu kompyuta za mezani 40 na kompyuta mpakato 16 hazijulikani zilipo baada ya wanafunzi kuvamia maeneo mbalimbali ya shule hiyo alfajiri ya kuamkia leo majira ya saa nane usiku na kufanya uiharibifu hio na kuvunja vinja vioo vya majengo na magari.

Chelsea yailaza Manchester City


Bao la ushindi na Ivanovi
Manchester City ilikuwa imeshinda mechi zote 11 ilizokuwa imecheza nyumbani kabla ya kukutana na Chelsea.
Kadhalika hii ndiyo imekuwa mara ya kwanza Manchester City kushindwa kufunga bao katika mechi za nyumbani tangu mwaka 2010.
Bao la Chelsea lilifungwa na Branislav Ivanovic katika kipindi cha kwanza .
Kocha Pellegrini wa ManCity
Kutokana na mechi hiyo Manchester City na Chelsea zina alama sawa lakini Mancity imefunga mabao mengi.
Liverpool iko katika nambari ya nne, Everton ni ya tano ilhali Tottenham ni sita huku Manchester United ikishikilia nafasi ya saba.
CHANZO:BBC
POSTED BY:Nasra Kimaro