Thursday, June 5, 2014
DK. BILALI ASHIRIKI SHEREHE ZA KUAPISHWA RAISI WA MALAWI
12:23 AM
No comments

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akimpongeza Rais mpya wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika baada ya
Rais huyo mpya wa Malawi kukabidhiwa madaraka jijini Brantyre kwenye
hoteli Sunbird. Baada ya kukutana viongozi hao walipata fursa ya
kuzungumzia masuala la kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili na
kukubaliana kuendelea kuwa na mahusiano mema kama nchi zinazoishi ndugu
na jirani. Picha kwa Hisani ya Ikulu ya Malawi

Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DkT. Mohammed Gharib Bilal leo
Jumatatu Juni 02, 2014 ameshiriki katika sherehe za kukabidhi madaraka
kwa Rais mpya wa Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika katika sherehe
zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu Banda jijini Blantyre. Sherehe
hizo pia zilihudhuriwa na Rais wa Botswana sambamba na wawakilishi wa
nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini na nyinginezo.
Akihutubia
baada ya kukabidhiwa sime ambayo ni ishara ya kuwa kiongozi wa watu wa
Malawi, Rais Mteule Mutharika alisisitiza kuwa, katika kipindi cha
utawala wake atahakikisha kuwa anaifanyia makubwa Malawi sambamba na
uhakikisha kuwa anaifanya Malawi itimize majukumu yake ya kimataifa
kufuatia kutambua kuwa kujitenga kunaweza kuifanya Malawi kutonufaika na
fursa zilizopo duniani.
“Nchi
hii ipo katika dunia na siyo rahisi tena kuwa na fikra kwamba Malawi
inaweza kubaki peke yake kama kisiwa. Tunahitaji kuwa na wenzetu wa
kusaidia maendeleo ya Malawi. Tunawahitaji wahisani toka Kusini ama
Mashariki, tunayahitaji mataifa tajiri na mataifa yanayoendelea.
Tutafanikiwa sana kama tutaendeleza urafiki kwa wote. Tufanye hivi bila
kujali kuwa sisi ni taifa kwani hali ya sasa inahitaji kila mmoja wetu
kushirikiana na mwenzake,” alisema.
Katika
hotuba hiyo pia amesisitiza kuwa kipindi chake cha utawala atajitahidi
kukabiliana na rushwa na kwamba hatakuwa na mchezo kwa wala rushwa
katika kipindi akiwa madarakani. Pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa
kuiunganisha Malawi kwa miundombinu bora ili kuboresha maisha ya
wananchi sambamba na kusogeza huduma za wananchi karibu.
Rais
Mutharika aliapishwa juzi baada ya kuwashinda washindani wake akiwemo
Rais aliyemaliza kipindi chake Joyce Banda ambaye hata hivyo hakuweza
kutokea katika sherehe hizi za kukabidhi madaraka. Akizungumzia suala la
kutohudhuria kwa Rais Banda, Rais Mteule Mutharika alisema alitegemea
Rais Banda kuwepo lakini hakufika nay eye anatambua kuwa wakati wa
uchaguzi kulikuwa na tofauti baina yao lakini kwa sasa uchaguzi umeisha
na amesahau yaliyopita ili kuanza ukurasa mpya wa kuijenga Malawi.
Katika shughuli hiyo pia Rais wa zamani wa Malawi Kamuzu Banda
alihudhuria.
Makamu
wa Rais Dkt. Bilal na msafara wake walitarajiwa kurejea nyumbani leo
hii Jumatatu mara tu baada ya kukamilika kwa kazi hii ya makabidhiano.
Wednesday, April 30, 2014
AJALI YA BASI LA SUMRY YAUA 22 WAKIWEMO POLISI WANNE...
1:59 AM
No comments
Gari
la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya
mkoa wa Singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa.
Moja
ya maiti ya ajali ya basi la Sumry iliyotokea katika kijiji cha Utaho,
Wilayani Ikungi mkoani Singida ikisubiri kupakiwa katika gari la polisi.Basi hilo la kampuni ya Sumry hufanya safari zake kati ya Kigoma na Dar-es-Salaam.
Dereva wa basi hilo alikimbia mara tu na baada ya ajali hiyo na kulitekeleza basi hilo.
Mwandishi wa habari wa ITV alifika na kuwakuta wasafiri walionusurika wakiwa katika kituo cha polisi cha Ikungi bila ya kujua hatima yao ya safari baada ya basi lao kuwakanyaga na kuuwa watu 22
Sudan Kusini kujadiliwa hatima yao kujiunga na EAC leo
1:56 AM
No comments
Mkutano wa mwisho kama huu uliofanyika mjini Kampala Uganda mwezi Novemba mwaka jana, uliweka bayana kwamba ni katika mkutano huuu wa Arusha, ambapo tarehe ya Sudan Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki itakapotangazwa.
Lakini wadadisi wanasema kuwa msukosuko wa kiuchumi pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe huenda ikawa sababu ya taifa hilo kunyimwa uanachama wa jumuiya hiyo. Hii ni baada ya machafuko ya wenyewe kwa
wenyewe kuzuka, na kusambaratisha nchi hiyo kisiasa na kiuchumi.
Maswala mengine yatakayojadiliwa ni ripoti ya mawaziri, mikakati ya kifedha katika kuiendesha jumuiya hiyo na mbinu za nchi wanachama kuendelea kupeana taarifa za kijasusi, katika juhudi za kupambana na tishio la ugaidi.













