NICE MEDIA WORKS

KWA WAIMBAJI WA INJILI

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, October 22, 2014

CHADEMA KUIPELEKA MAHAKAMANI KATIBA ILIYOPENDEKEZWA ISIPIGIWE KURA NA WANANCHI


Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimesema kinakamilisha ushahidi ili kwenda mahakamani kupinga katiba inayopendekezwa kupelekwa katika hatua ya kupigiwa kura ya maoni kwa madai kuwa katiba hiyo imekosa uhalali kutokana na kukosa theluthi mbili kutoka upande wa Zanzibar.
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara Profesa Abdalah Safari ametoa tamkoa hilo wakati akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake kwenye uwanja wa Mlandege ambapo amebainisha kuwa zoezi la kupitisha rasimu ya katiba inayopendekezwa ndani ya Bunge maalumu la katiba liligubikwa na mbinu chafu za uchakachuaji wa kura hasa za wajumbe wa Zanzibar.
 
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho Dokta Wilbrod Slaa amesema chama cha mapinduzi kimeanza kuhujumu mchakato wa uandikishaji wa wananchi kwenye Daftarai la Makazi kwa kuendesha zoezi hilo kwa siri huku kikitumia mabalozi wa nyumba kumi wa chama hicho kinyume na utaratibu wa kawaida ambapo kazi hiyo inapaswa kufanywa na watendaji wa vijiji kata na mitaa.
 
Aidha katibu mkuu huyo wa Chadema amewataka wananchi kutodanganyika na vipengele vya haki za makundi mbalimbali zilizowekwa kwenye katiba hiyo pendekezwa akieleza kuwa zimewekwa kama chambo kwani haki hizo zimeondolewa na kifungu cha 21 kinachoeleza kuwa haki hizo hazitadaiwa mahakamani

Tuesday, October 7, 2014

UJASIRIAMALI NI MKOMBOZI WA MAISHA..ARUSHA

Mkurugenzi wa mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha bwana Joseph Mayagila Akifungua semina ya ujasiriamali iliyofanyika chuoni hapo hivi karibuni...
habbari na Yasinta Peter
Wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wametakiwa kujishughulisha na biashara pamoja na kuwa na tabia ya kujiwekea akiba kwa ajili ya maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa chuo hicho Bw.Joseph Mayagila  wakati akifungua semina ya ujasiriamali ambayo ilifanyika kwa siku tatu chuoni hapo kuanzia tarehe 1 mpaka tarehe 3 Octoba mwaka huu chuoni hapo.

Bw.Mayagila ameongeza kuwa wanafunzi wengi hawana tabia ya kujiwekea akiba katika fedha ambazo wanatumiwa na wazazi wao kwa ajili ya matumizi na kuwaasa wanafunzi hao wawe wanajiwekea akiba kwa maendeleo yao.

Katika semina hiyo walimu wa chuo hicho waliyoa mada mbalimbali zikiwemo za mpango wa biashara,miongozo ya mjasiriamali,namna ya kutathmini biashara pamoja na nyingine nyingi ambapo wanafunzi wote wa chuo hicho walishiriki.

Pia ili kuongeza vionjo katika semina hiyo kulikuwepo na  burudani mbalimbali ambapo wanafunzi walipewa fursa ya kuonyesha vipaji vyao mbele wanafunzi wenzao na burudani hizo ni pamoja na kuimba pamoja na vichekesho.

Nao wanafunzi wa chuo hicho wamesema kuwa wamefurahishwa na uwepo wa semina hiyo kwa sababu imewafunza mambo mbalimbali juu ya ujasiriamali ambayo hawakuwa wakiyafahamu.

Mmoja wa wanafunzi hao Bi.Edna Lucas alikuwa na haya ya kusema,
‘’Semina ni nzuri na nimeweza kujifunza mambo mengi ambayo sikuwa nayajua na kwa kupitia semina hii nimehamasika kufanya biashara’’.

Akizungumza ili kuhitimisha semina hiyo makamu mkuu wa chuo Bw.Elifuraha Samboto amewataka wanafunzi  kuwaheshimu walimu na vilevile wawe na tabia ya kjisomea.

Bw.Samboto alimaliza kwabkuwashukuru walimu na wanafunzi kwa ushiriki wao katika semina ya jasiriamali.

Thursday, September 25, 2014



WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, amewataka Watanzania kuacha kununua bidhaa zisizosindikwa kwani hupunguza pato la taifa na kuchangia kupungua kwa ajira nchini.

Alisema hayo jana katika ufunguzi wa maonesho ya bidhaa kutoka China, ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya wanunuzi wa bara la Afrika.

Alisisitiza kuwa, urafiki wa Tanzania na China unaimarika kutokana na juhudi mbali mbali zinazofanywa na serikali zote mbili hasa katika biashara.

“Tumezungumza na Serikali ya China kuona ni namna gani itaweza kutusaidia kutatua changamoto kubwa zinazotokana na uchumi, kwani wenzetu (China) wako mbele kimaendeleo zaidi yetu,” alisema Dk. Kigoda.

Akizungumzia changamoto ya kuingizwa kwa bidhaa zisizo bora kutoka uchina Dk. Kigoda, alisema serikali inashindwa kudhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu ambao hushiriki vitendo hivyo kutokana na wingi wa mipaka inayoizunguka nchi na kukosa watendaji wa kutosha katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Aidha, Balozi wa China nchini Lu Youqing, alisema Watanzania wanakaribishwa kutangaza bidhaa nchini China katika kukuza soko la bidhaa zao.

“Kwa sasa bidhaa za Uchina zinauzwa kwa bei nafuu ili kuendana na hali ya kimaisha ya Watanzania wengi katika kusaidia upatikanaji wake bila kubagua hali ya mtu,” Alisema Balozi Youqing.

Maonyesho haya yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam jana, yataendelea kufanyika hadi mwishoni mwa wiki hii nia ikiwa ni kutoa fursa kwa Watanzania kufahamu bidhaa zinazozalishwa kutoka China. 




Habari na Everline bakari,

CHADEMA KILOSA WABAINI MCHEZO MCHAFU


 
UONGOZI mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jimbo la Kilosa mkoani Morogoro umeanza kazi kwa kunasa makada wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Magomeni wilayani hapa wakiwa na nyaraka za serikali kinyume cha sheria wakiandikisha majina ya watu.

Wakizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Kilosa, Seleman Simba na Katibu wa Jimbo la Kilosa Kati, Mussa Ngongi, kwa nyakati tofauti walisema makada hao wa CCM waliwanasa Septemba 7 mchana wakiendelea na zoezi hilo la uandikiashaji.

“Kisheria zoezi lilipaswa kufanywa na maofisa watendaji wakishirikiana na wenyeviti wa vitongoji, tofauti na hivyo uongozi wa halmashauri kwa makusudi umegawa kwa makada wa CCM vitabu vya kuandikisha majina ya wakazi vitongoji…kwa mtazamo wetu hii inafanyika makusudi kuiandalia CCM ushindi katika chaguzi zijazo,” alifafanua Ngongi.

Viongozi hao, walisema mbali na zoezi hilo kushitukiwa kwa kupewa makada wa CCM kuliendesha badala ya watumishi wa serikali, walilishitukia kutokana na lilivyokuwa likiendeshwa kwa ubaguzi likiwatenga wenye itikadi tofauti na CCM na wenye misimamo tofauti.

Walibainisha kuwa kilichowashangaza zaidi ni hata baada ya suala hilo kufikishwa kituo kikubwa cha polisi wilayani hapa, Polisi akiwemo mkuu wa kituo hicho walilazimisha suala hilo kumalizwa kwa mazungumzo badala ya sheria kufuta mkondo wake.

Katika ufafanuzi wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Idd Mshili, mbali na kukiri kuwepo kwa zoezi la utambuzi wa wakazi unaofanyika kila baada ya miezi mitatu, alikana halmashauri hiyo kutoa kazi hiyo kwa makada wa CCM zaidi ya maofisa watendaji anaowatambua kisheria.HABARI  NA  WINLADY  JOHANESS

UTATA KESI YA KUBENEA KUPINGA BUNGE MAALUM




KESI ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari, Said Kubenea akihoji mamlaka ya Bunge la Katiba, jana imeibua utata baada ya majaji kubaini maana mbili tofauti ya kifungu cha 25(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2011.

Mmoja wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji Aloysius Mujulizi alibaini hilo wakati Kubenea akiwasilisha hoja zake kupitia kwa mawakili wake, Peter Kibatala na Mabere Marando katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Majaji w
engine wanaounda jopo hilo, linalosikiliza kesi hiyo ni Augustino Mwarija na Dk Fauz Twaib. Jaji Mujulizi alisema kuna utofauti wa maana ya kifungu hicho katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili, jambo lililosababisha Kibatala asome kifungu hicho kilivyoandikwa kwa lugha hizo. Katika Kiswahili kifungu hicho kimeandikwa:

“Mamlaka ya Bunge Maalumu ya kupitisha masharti ya Katiba yanayopendekezwa, yatatekelezwa baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na kupitishwa na Bunge.”
Wakati kwa tafsiri ya Kiingereza, imeandikwa Bunge Maalumu la Katiba litatekeleza madaraka yake kwa kuongozwa na kujikita kwenye Rasimu itakayokuwa imewasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na kupitishwa na Bunge.
Wakili Marando alidai jambo hilo, linatokana na Kiingereza kibovu na kutoandikwa kwa ufanisi, lakini licha ya upungufu huo bado bunge hilo linatakiwa kufanyakazi kwa mujibu wa misingi ya rasimu ya Katiba
.
Aidha, hakuna kifungu chochote kinachoruhusu bunge hilo kutofuata rasimu, pia halina mamlaka ya kukusanya maoni mapya, wakifanya hivyo watakuwa wanakwenda kinyume na maoni ya wananchi, lakini wajumbe hao wanakusanya maoni yao na hivi karibuni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta aliwaita watu watoe maoni yao.

Kibatala aliiomba Mahakama itoe tafsiri ya kifungu hicho, kwasababu kutokana na mgongano wa tafsiri hiyo, taifa limegawanyika na hata wajumbe wa bunge hilo wametengana.

Alidai kundi moja la wajumbe la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), limegoma kuendelea na vikao hivyo, wakati kundi linaloendelea na vikao linakusanya maoni mapya, kwa madai kifungu hicho kinawapa mamlaka.
Akijibu hoja hizo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alidai kuwa vifungu hivyo, havitofautiani kwa kuwa vinaleta maana moja, lakini kuna tatizo la maandishi na matumizi ya lugha.

Aliongeza kuwa Bunge lilipewa rasimu kama nyaraka ya kufanyia kazi na hakuna ulazima wa kufuata kifungu hicho. Kubenea alifungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiomba Mahakama itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba, kwa kuzingatia Kifungu cha 25 (1) na (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2011.

Aidha, anaiomba Mahakama itamke kama bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba, iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.HABARI  NA  WINLADY  JOHANESS

POLISI WAZUIA MKUTANO CHADEMA, WARUHUSU CCM


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa MomboBAADHI ya wananchi wa Mji wa Mombo wamedai, hawajafurahishwa na Jeshi la Polisi mjini hapa, kuzuia mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kuruhusu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.

Kwa mujibu wa wananchi hao, walidai kuwa Polisi jana ilizuia kutoa kibali kwa CHADEMA iliyoomba kufanya Mkutano katika Mji Mdogo wa Mombo Ijumaa ijayo kisha kuruhusu CCM ifanye mkutano katika mji huo.

Polisi mmoja ambaye hakutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo, alikiri kuwa chadema wamenyimwa kibali kwa kuwa wameomba maandamano na mkutano.
“CHADEMA walizuiwa kwa sababu waliomba Kibali cha Maandamano na Mkutano, hivyo kwa kuwa maandamano yamepigwa Marufuku nchi yote, hawakuruhusiwa kufanya hivyo na kwamba kitendo cha kufanya hivyo bila kibali, watalazimika kuwatawanya.

“Ni kweli CCM wamekubaliwa kufanya Mkutano hapa Mombo Ijumaa, Septemba 26, utakaohutubiwa na Kinana, na CHADEMA tuliwaruhusu kama wanataka kufanya Mkutano wafanye Mombo, Septemba 26, lakini si Maandamano”, alisema.

Mwenyekiti wa CHADEMA Korogwe, Aurelian Nziku, alisema kuwa waliomba kibali cha kufanya maandamano ya amani na mkutano ila polisi imezuia maandamano na kuruhusu mkutano wa CCM, ila wao pia wameruhusiwa kufanya mkutano mwishoni mwa wiki.HABARI  NA  WINLADY   JOHANESS

JUMUIYA YA WATUMIAJI MAJI NZIHI WAPATIWA PIKIPIKI

 

 
MKURUGENZI wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Kampuni ya Simu Tigo, Jackson Kiswaga ametoa msaada wa pikipiki kwa jumuiya ya Watumiaji Maji Kata ya Nzihi kwa lengo la kumaliza kero iliyokuwa inawakabili ya usafiri ili kuwawezesha kutembelea mitambo mbalimbali kwa urahisi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika hivi karibuni katika ofisi za kata hiyo, Kiswaga aliahidi kuendelea kushirikiana na wananchi katika kuwaletea maendeleo.

Alisema apatapo fursa ya kukutana na watu wa ndani na nje ya nchi wanaoweza kusaidia maendeleo ya watu wengine amekuwa akiyakumbuka matatizo ya wananchi wa Iringa na kuomba msaada.

“Hakika katika kuleta maendeleo nitahakikisha nashirikiana na wenzangu katika maendeleo yetu, sitaacha kutoa mchango wangu, nimefanya hivyo muda mrefu uliopita, nafanya hivi sasa na nitaendelea kwa siku zijazo,  nimekutana na wadau kutoka Marekani, Ulaya na Afrika Kusini kuna mambo yanakuja katika sekta ya afya na elimu na yatakapokuwa tayari nitawaleta ,”  alisema Kiswaga.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Steven Mhapa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nzihi, alisema chombo hicho cha usafiri kitaiwezesha jumuiya hiyo kusafiri eneo moja hadi lingine kufuatilia maendeleo na changamoto zinazoukabili mradi huo wa maji.

Naye Meneja wa Watumiaji Maji Kata hiyo, Ha
mza Chorobi, alisema mradi huo wa maji una changamoto kama vile uchakavu wa miundombinu yake na ongezeko la watumiaji wa huduma hiyo, hivyo unahitaji zaidi ya sh milioni 300 kwa ajili ya ukarabati.HABARI  NA  WINLADY   JOHANESS