Thursday, July 3, 2014

Ridhiwani Kikwete amudu kikaango

Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhwani Kikwete leo hii imekuwa ni zamu yake kushiriki kuchat Live na wananchi pamoja na wafuasi wake kupitia Kikaangoni Live ya ukurasa wa Facebook wa EATV, ambao unahusisha familia kubwa kabisa ya mashabiki.

Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete, kupitia ukurasa wetu wa Facebook ameweza kuelezea mambo mbalimbali yanayomhusu wakati akijibu maswali ya mashabiki wake katika ulingo wa siasa na kama mtoto wa Rais.

Ridhiwani amekiri kupata maswali mengi ambayo yamekuwa changamoto kwake ambapo yamemlenga kwa namna moja au nyingine kuhusiana na ulingo wa siasa na pia hakuacha kutoa pongezi zake kwa msanii Diamond ambaye aliiwakilisha nchi alipokuwa "nominated" katika tuzo za BET zilizofanyika hivi majuzi nchini Marekani.

Zoezi hili linafanyika kila Jumatano saa 6 mpaka saa 8 mchana kupitia www.facebook.com/eatv.tv, Like ukurasa huu kama bado hujafanya hivyo ili kuwa sehemu ya familia hii kubwa, na kaa tayari kwa staa mwingine mkali kupitia Kikaangoni Live wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment