Wednesday, December 4, 2013

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUJENGA MAZOEA YAKUJISOMEA VITABU MBALIMBALI!!

Mkurugenzi wa redio faraja Bw.Simeo Makoba akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari na Utangazaji.


Mkurugenzi wa kituo cha redio faraja Bw.Simeo Makoba amewataka waandishi wa habari kujenga mazoea ya kujisomea vitabu pamoja na kusikiliza vyombo mbalimbali vya habari ili kujua taarifa zinazoendelea hapa nchini na nje ya nchi.

Bwana Makoba aliyasema hayo Mkoani Arusha alipokuwa akizungu mza na waandishi wa habari katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) kwalengo lakuwaimarisha kinadharia.
Akitoa ufafanuzi juu ya taaluma ya habari Bw.Makoba amesema nivema wanahabari kujitambua ikiwa ni pamoja na kuweka jitihada katika masomo yao kwa nadharia na vitendo.
Bw.Makoba alisema”Waandishi wa habari ni watu wanaotakiwa kuwa wadadisi,wafuatiliaji wa mambo pamoja na kuyafichua yale yote yanayolenga kuikandamiza jamii pamoja na unyanyasaji”alisema Bw.Makoba
Aliendelea kusema kuwa Ufanisi wa kazi katika tasnia ya habari umekuwa na changamoto nyingi ambazo  zipo baadhi yake zinazosababishwa na waandishi wenyewe na pia zipo zinazochangiwa na serikali.
 Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kutodhaminiwa, kutokupata maslahi yakutosha, vitisho vya kipigo, kutokuwa na ulinzi pamoja na uwezeshwaji kwa wanahabari.
Hatahivyo ametoa wito kwa wanahabari kuwa na muonekano mzuri kwa jamii pamoja na kuvaa mavazi yanayosadifu kazi yao, pamoja na kufanya kazi ipasavyo ili kuijenga taaluma ya uandishi wa habari.
By Virginia Daniel & Emmanuel Ndanshau.

0 comments:

Post a Comment