Mkurugenzi wa mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha bwana Joseph Mayagila Akifungua semina ya ujasiriamali iliyofanyika chuoni hapo hivi karibuni...
habbari na Yasinta Peter
Wanafunzi wa
chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wametakiwa kujishughulisha na
biashara pamoja na kuwa na tabia ya kujiwekea akiba kwa ajili ya maendeleo.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa chuo hicho Bw.Joseph Mayagila wakati akifungua semina ya ujasiriamali
ambayo ilifanyika kwa siku tatu chuoni hapo kuanzia tarehe 1 mpaka tarehe 3
Octoba mwaka huu chuoni hapo.
Bw.Mayagila
ameongeza kuwa wanafunzi wengi hawana tabia ya kujiwekea akiba katika fedha
ambazo wanatumiwa na wazazi wao kwa ajili ya matumizi na kuwaasa wanafunzi hao
wawe wanajiwekea akiba kwa maendeleo yao.
Katika
semina hiyo walimu wa chuo hicho waliyoa mada mbalimbali zikiwemo za mpango wa biashara,miongozo ya
mjasiriamali,namna ya kutathmini biashara pamoja na nyingine nyingi ambapo
wanafunzi wote wa chuo hicho walishiriki.
Pia ili
kuongeza vionjo katika semina hiyo kulikuwepo na burudani mbalimbali ambapo wanafunzi walipewa
fursa ya kuonyesha vipaji vyao mbele wanafunzi wenzao na burudani hizo ni
pamoja na kuimba pamoja na vichekesho.
Nao
wanafunzi wa chuo hicho wamesema kuwa wamefurahishwa na uwepo wa semina hiyo
kwa sababu imewafunza mambo mbalimbali juu ya ujasiriamali ambayo hawakuwa
wakiyafahamu.
Mmoja wa
wanafunzi hao Bi.Edna Lucas alikuwa na haya ya kusema,
‘’Semina ni
nzuri na nimeweza kujifunza mambo mengi ambayo sikuwa nayajua na kwa kupitia
semina hii nimehamasika kufanya biashara’’.
Akizungumza
ili kuhitimisha semina hiyo makamu mkuu wa chuo Bw.Elifuraha Samboto amewataka
wanafunzi kuwaheshimu walimu na vilevile
wawe na tabia ya kjisomea.
Bw.Samboto
alimaliza kwabkuwashukuru walimu na wanafunzi kwa ushiriki wao katika semina ya
jasiriamali.